Serikali ya Urusi imeipiga marufuku kampuni nguli ya mitindo inayofahamika duniani kote kwa kuwa na bidhaa za ngozi za viwango na bei kubwa kama mabegi na vitu ya Louis and Vuitton au maarufu kama kifupisho chake cha LV. Marufuku hiyo ya serikali ya Urusi ilisababishwa na kampuni hiyo ilijenga "banda" lenye ukubwa wa mita za mraba 34 lenye umbo la sanduku kubwa la LV kwa lengo la kutangaza bidhaa zake kwa wakazi wa mji huo na nchi hiyo. mara baada ya kujengwa kwa banda hilo katikati ya uwanja maarufu na wa kihistoria wa Red Square, watalii ambao kwa kawaida walikuwa wakienda katika uwanja huo wa kumbukumbu za kisiasa wa Red Red Square, ambapo pia ipo kumbukumbu ya kiongozi aliyeongoza mapinduzi ya kisiasa na baba wa taifa hilo Vlamidir Lenin, tokea kuwekwa kwa sanduku hili la maonyesho wamekuwa wakipiga picha hapo na kusababisha kejeli kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Urusi kuwa LV ni kifupi cha baba wa Taifa wa nchi hiyo yaani Lenin, Vlamidir.
Wasemaji wa kampuni ya Louis Vuitton wamesema kuwa hawapo katika nafasi ya kuzungumizia kampeni hiyo ya utata, ila mtu wa karibu na wasemaji wa kampuni hiyo amesema kuwa inasikitisha kuwa haijapoklewa vizuri na serikali nchini humo kwani lengo la tangazo hilo ilikuwa ni kuvutia watu kuchangia watoto katika kampeni inayoratibiwa na NataVodyanova, mwanamitindo na rafiki wa mtoto wa Bernard Arnault, anayeongoza kampuni hiyo ya LV.
Angalia picha ya banda hilo ikiwa imeipa muonekano tofauti uwanja wa Red Square.
No comments:
Post a Comment