Pages

Monday, December 16, 2013

DONT TRY THIS AT HOME PLEASE!!!!

Prem Singh amekuwa kivutio kikubwa anapokuwa katika kazi yake ya upishi

anaonekana akitumbukiza mkono wake katika kikaangio cha mafuta ya moto bila kuathirika kwa namna yoyote

Akiendelea kuonyesha kipaji uwezo wake huo, Nimechanganyikiwa hapa ni kipaji hiki, mazingaombwe au uwezo..???

kiwe kidole kimoja, vidole vingi, mkono mzima mwisho wa siku haungui hata kiduchu kidogo lol!!!!

Hapa anaonekana akiwa katika duka lake linalouza maakuli moja kwa moja toka jikoni.

Duka lake linayoonekana kwa nje, alirithi kazi hii kutoka kwa baba yake, sehemu ya Old Delhi tangu mwaka 1960
Singh said: 'Everyone wants me to dip my hand into hot oil. They want to see how I do it.'
Singh's father started the small shop called Ganesh in Old Delhi in 1960.
Katika duka lake hilo lililojipatia umaarufu maeneo hayo, Bw. Singh amekuwa akiuza samaki wa kukaanga lakini pia napika vitafuni vingine vyenye asili ya kihindi kama kababu na kuku aina ya tandoori, anasema kuwa kwa siku huweza kuuza mamia ya kilo za samaki kwa wateja mbalimbali kutokana pia na wateja wengi wanaokuja kuona namna anavyotumia mikono yake kupika kwa kuitumbukiza ndani ya kikaango cha mafuta ya moto ambayo hufikia nyuzi joto 200!!!!!

Anasema pia kuwa huweza kupata wateja hata kutoka nje ya mji anaoishi kwa ajili ya kuja kuona na kuonja ladha ya mapishi yaho tunayoweza kuyaiota ya ajabu., mmoja wa wateja wake wa kila siku Bw. Dipesh anasema kuwa yeye huwa anakuja mara kwa mara na anapofika tu Delhi, kitu cha kwanza anachofanya ni kuja kuonja samaki hao..." huwa nashangazwa sana na namna bwana huyu anavyotumbukiza mkono wake kutoa samaki au kugeuza samaki wakiwa kikaangoni, ni ngumu kueleza au kuamini hadi unaposhuhudia kwa macho yako mwenyewe, lakini pamoja na maajabu ya kutumia mikono yake, pia kuna ladha ya pekee kabisa unapoonja samaki wake"


Watoto wawili wa Bw. Singh sasa wanashirikishwa na baba yao katika biashara hiyo, mtoto mkubwa Deepak anasema kuwa na wao wamejiunga katika bishara hiyo ya familia ambayo babu yao na baba yao wameianzisha. Wanaendelea kueleza kuwa wao wanataka kuiboresha zaidi ili iwe kubwa bna bora zaidi. Naye Bw. Singh anatumaini kuwa watoto wake watadumisha utamaduni wa kukaanga kwa kutumia mikono...anasema " wanaweza kabisa kuifanya, wanachohitaji ni kujizoesha tu, wakieendelea kujaribu watazoea na mwisho wataweza kufanya kama mimi ninavyofanya" Mhhhh!!! haya baba tumekusikia....ni kazi rahisi sana kutumia mkono badala ya mwiko katika kikaangio cha mafuta.....;-)

No comments:

Post a Comment