Habari za kusikitisha kutokana na taarifa hizi, jina hili so geni na hasa kwa kwa wale wanaofuatilia sana mbio za magari za Forular One na nyinginezo, ambapo mshindi wa mara nyingi wa mbio za magari za formular One wa Ujerumani Michael Schumacher yupo mahututi na akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata ajali wakati akiwa katika mchezo a kuteleza katika barafu na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 14 anayeita Mick.
Schumacher mwenye umri wa miaka 44, alijiuzulu katika mashindano hayo ya magari ya F1 akiwa amejipatia heshima ya dereva bora kabisa ambaye hajawahi kutokea na akiwa ameshinda mara saba taji hilo, inasemekena ameumia kutokana na ubongo wake kuvuja damu na alikuwa amevaa helmet wakati alipopata ajali hiyo alipoenda kugonga katika jiwe kubwa wakati akiteleza kwenye barafu katika safu za milima ya Alps iliyopo Ufaransa huko Maribel.
|
akiwa na mwanaye Mick mwenye umri wa miaka 14 aliyekuwa naye ajali ilipotokea |
|
akiwa na mkewe Corrina |
|
akiwa katika mchezo huo wa kuteleza katika barafu uliosababisha ajali husika |
No comments:
Post a Comment