Madaktari huko China wamefanikiwa kuunganisha mkono uliokatika wa majeruhi wa ajali na kuunganisha katika mguu wake ikiwa ni katika jiihada za kuufanya mkno huo uweze kutumika tena hapo baadaye pale utakaporudishiwa mahali ulipokatikia. mnamo November 10, 2013 Xiao Wei alikatika mkno sehemu ya juu kidogo ya kiganja baada kupata ajali akiwa kazini na anasema kuwa mara baada ya mashine kuukata mkono wake, wafanyakazi wenzake walizima mashine na kuuokota mkono kisha kumuwahisha hospitali ..." sikuweza kusikia maumivu wala kufanya chochote , hakika nilikuwa katika mshtuko mkubwa"
Mmoja wa madaktari hao analeza kuwa majeraha yake yalikuwa ni makubwa sana, pamoja na kukatika, mkono huo pia ulikuwa umekandamizwa na mashine na kuwa bapa kabisa, hivyo ilibidi kwanza kuyatibu majeraha yake kabla ya kuurudishia mkoo katika sehemu yake. Wanaendelea kueleza kuwa baada ya kutibiwa kwa mwezi mzima, tuna uhakika Xiao, anaweza kufanyiwa upasuaji wa kurudishiwa mkono wake kwa mafanikio.
|
Kipande cha mkono kikiwa kimeshonelewa katika mguu wa Xiao ili baadaye kiondolewe na kushonewa mahali ulipokatikia |
|
daktari akiwa na mgonjwa tayari kwa kuondoa kipande cha mkno ili kuweza kurudishiwa sehemu husika. |
|
Kipande cha mkono kikiwa tayari kimerudishiwa katika kiwiko kilipokatikia. |
No comments:
Post a Comment