Pages

Monday, December 30, 2013

FROM MY BACKYARD

Nakumbuka hivi viazi miaka ya nyuma vilikuwa so popular and all over the place, tulikuwa tunapenda kuviita viazi vya njano au viazi karoti na utamu wake ulikuwa ni balaa, kulinganisha na viazi vingine. Baadaye vikawa vimepotea kabisa sokoni hata uienda inakuwa ni kwa kubahatisha na halafu huwezi kuvipata vingi. Juzijuzi pia katika vyombo vya habari nmesikia kampeni ya kuhamasiha wakulima kuvipanda viazi hivi kwani vina ubora wa kilishe na hata kibiashara kulinganisha na vilivyopo. So ilitokea kwa bahati nilipata mbegu za viazi hivi kibahari tu kwani mm nilitaka kwa ajili ya matembele ndio nikapewa na baada ya kupanda kwenye kaeneo kadogo sana sikuwa   hata na matarajio yoyote ya viazi maana mm shida ilikuwa ni matembele, kweli mvua zikanyesha na baada ya muda kupita tukashangaa kuona vimetutumka kwa juu ya ardhi, yaani kwenye mashindna yaliyokuwa hayafiki hata matano tulipata viazi vikubwa na vya kutosha kabisa..#happyface# so next year, um ... in few days to come nitavipanda kwa wingi mvua tu zikianza ili nivipate kwa wingi..#kilimokwanza#

Viazi vitamu vikiwa shambani

 


nilivyovivuna bustanini kwangu vikiwa vimeandaliwa kwa kukaangwa....


No comments:

Post a Comment