Pages

Sunday, December 1, 2013

MUIGIZAJI WA FILAMU ZA FAST AND THE FURIOUS AFARIKI DUNIA

Muigizaji katika filamu maarufu za Fast and Furious nchini Marekani, mbaye katka filamu hizo aliigiza kama mpelelezi Brian O'Conner amefariki dunia. Mwigizaji huyo alipoteza maisha baada ya kupata ajali mbaya tarehe 3o November katika jiji la California. kwa kipindi hiki alikuwa yupo katika maandalizi ya sehemu nyingine ya filamu hizo za Fast and the Furious katika mji wa Atlanta, kabla ya ajli hiyo iliyotokea katika wakati akiwa anarudi kutoka California alikoenda kuhudhuria onyesho la hisani jijini humo.

mwigizaji huyo anayejulikana kwa jina la Paul Walker  wakati ajali hiyo inatokea alikuwa ni abiria katika gari aina ya Porsche Carrera GT iliyokuwa inaendeshwa na rafiki yake wa siku nyingi, Roger Rodas, lilipoteza  mwelekeo na likiwa katika mwendo na kwenda kugonga nguzo ya taa katika eneo la Valencia, magharibi mwa mji wa Los Angeles. Polisi walipofika katika eneo la tukio la ajali hiyo, walikuta gari ikiwa inawaka moto huku kukiwa na watu wawili ndani yake ambapo walitangaza kuwa wamefariki mara tu baada ya ajali hiyo kutokea, muigizaji huyo, Paul, amefariki akiwa na umri wa miaka 40 tu.
 
Paul Walker
 
 
wakati wa uhai wake


walker banner
gari inavyoonekana baada ya ajli hiyo.

No comments:

Post a Comment