Lakini baada ya kupachimba, mahala hapo palitumbukia ndani na kuacha shimo kubwa na pana ambapo pia badala ya mafuta waliyotegemea kuyapata walikutana na gesi aina ya methane ambayo waliamini kuwa wangeiacha iendelee kuvuja hewani ingesababisha madhara makubwa kwa watu waliokuwa wanakaa maeneo ya jirani. Hivyo ilibidi waache kuchimba shimo hilo na kuamua kulichoma kwa kuwasha moto ambao waliamini ungenguza gesi hiyo na kupaacha mahala hapo pakiwa salama na pakiwa hapana tena mvujo wa gesi. Kinachostaajabisha ni kuwa tokea wataalamu hao walipopachoma moto mahala hapo mwaka 1971 hadi leo panaendelea kuwaka moto, na kuwa kivutio kikubwa cha watalii wanaotoka mbali kuja kushuhudia eneo hilo ambalo wenyeji wamelipachika jina la 'milango ya kuzimu' moto huo unaendelea kuwaka huku kukitoa pia na matope ya moto na miale ya moto usioisha hadi sasa.
Tazama picha hapo chini............
shimo hilo lililobatizwa mlango wa kuzimu likionekana kwa mbali
miale ya moto isiyoisha ikitoka ikionekana katika shimo hilo
picha ya shimo kwa karibu
No comments:
Post a Comment