Pages

Saturday, November 23, 2013

SHIMO HUKO URUSI LAENDELEA KUWAKA KWA MIAKA ZAIDI YA 40........

Wnasayansi waliokuwa wanatafuta mafuta katika jangwa la Karakam katika eneo la Derweze, Turkmenistan, iliyokuwa chini ya Urusi ya zamani kama kawaida katika taratibu za utafutaji wa gesi ardhini walilitambua eneo ambalo waliamini lilikuwa na akiba kubwa ya mafuta. Hicho ndicho  kilichowafanya  wataalamu hao kuchimba kuelekea chini zaidi kwa vifaa maalumu ili kupata mafuta yaliyoaminika kuwa chini ndani ya eneo hilo.

Lakini baada ya kupachimba, mahala hapo palitumbukia ndani na kuacha shimo kubwa na pana ambapo pia badala ya mafuta waliyotegemea kuyapata walikutana na gesi aina ya methane ambayo waliamini kuwa wangeiacha iendelee kuvuja hewani ingesababisha madhara makubwa kwa watu waliokuwa wanakaa maeneo ya jirani.  Hivyo ilibidi waache kuchimba shimo hilo na kuamua kulichoma kwa kuwasha moto ambao waliamini ungenguza gesi hiyo na kupaacha mahala hapo pakiwa salama na pakiwa hapana tena mvujo wa gesi. Kinachostaajabisha ni kuwa tokea wataalamu hao walipopachoma moto mahala hapo mwaka 1971 hadi leo panaendelea kuwaka moto, na kuwa kivutio kikubwa cha watalii wanaotoka mbali kuja kushuhudia eneo hilo ambalo wenyeji wamelipachika jina la 'milango ya kuzimu' moto huo unaendelea kuwaka huku kukitoa pia na matope ya moto na miale ya moto usioisha hadi sasa.

Tazama picha hapo chini............

shimo hilo lililobatizwa mlango wa kuzimu likionekana kwa mbali




miale ya moto isiyoisha ikitoka ikionekana katika shimo hilo


picha ya shimo kwa karibu

No comments:

Post a Comment