Pages

Tuesday, March 25, 2014

"SELFIES" ZINAPOPITILIZA

kijana Danny Bowman wa nchini Uingereza ameifanya selfie kuwa hatari ambayo ingeweza hata kuhatarisha maisha yake pale alipotumia muda wake mwaingi kwa siku akichukua picha hizo na kuhakikisha kuwa anapata iliyo bora kabisa na isiyo na kasoro yoyote ile, ambapo kuna siku aliweza kutumia hadi saa kumi kwa siku akiwa anaweka mapozi mbalimbali ili kupata picha iliyo bora kabisa u maarufu kwa jina la selfie
kijana Danny Bowman

Tatizo hili lilianza akiwa na miaka 15 na ililimfanya aache shule na kupoteza uzito ambapo mama yake Penny alijaribu kumsaidia bila mafanikio yoyote, hadi alipotafuta msaada wa wataalamu wa magonjwa ya akili na sasa anaendelea na matibabu ambayo wataalamu wameyapa jina la OCD and  Body dysmorphic disorder (wasiwasi uliozidi kuhusu muonekano wa mtu)




akiwa na daktari wake alipokuwa akihojiwa kuhusu tatizo lake katika kipindi cha televisheni
Kabla ya kuanza kupata matibabu hayo alishwahi jaribu kujiua kwa kunywa vidonge vingi na pia kwa wakati fulani aliweza kukaa ndani ya nyumba yao kwa muda wa miezi sita bila kutoka nje hata kidogo.



No comments:

Post a Comment