Mchezaji maarufu wa mpira wa miguu Lionel Messi ameungana na watu maarufu akiwemo Abromavich, Sherly Cole na wengine ambao tayari wameupanda mlima maarufu nchini na duniani kwa ujumla Kilimanjaro maalumu kwa ajili ya tangazo linaloonyesha sehemu ambapo shirika la ndege la Turkish linafanya safari zake duniani. Tanzania ikiwa ni moja ya sehemu ambazo shirika hili linafnya safari zake nayo ilikuwa sehemu ya tangazo hilo. Wazo la tangazo hilo linatawaliwa na maneno maarufu sana kwa sasa pengine kuliko chochote katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii...yes, i mean #photobomb# and #selfie# ni kuwa Messi na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant wanashindana kupiga picha bora zaidi aina ya selfie. Tangazo linaanza kwa Messi kumtumia picha Kobe yake mwenyewe akiwa mbele ya kanisa la Saint Basil’s Cathedral mjini Moscow. Kobe naye anajibu mapigo kwa kwenda kwenye kuta maarufu za China (The Great Wall of China) na mashindano yanaendelea hadi kumfanya Messi aje kuchukua selfie kwenye mlima Kilimanjaro, huku maeneo yote hayo yakifikika na ndege za Turkish Airlines. Mwisho Messi anajipiga picha akiwa Sultanahmet Square mjini Istanbul, na kuja kugunduaa nyuma yake alikuwepo Kobe aliyetokea pia kwenye picha yake.
No comments:
Post a Comment